Usiku wa February 23 2016 Producer Mtanzania Lamar alipost video akiwa studio kwake na spika zikitoa mdundo mmoja mkali alafu akaandika caption yenye swali, watu wacomment kumwambia Msanii gani atafaa kupita juu ya huo mdundo kisha akamtag producer Scott Storch kwamba ndio anampa Inspiration, yani kazi ya Scott inamvutia na anajifunza vingi kutoka kwake.
Kabla ya yote inabidi ufahamu kwamba Scott Storch (42 yrs) ni producer maarufu wa Marekani ambaye mikono yake ilihusika kuzitengeneza beats za hits nyingi ikiwemoNaughty Girl ya Beyonce, Sorry ya Rick Ross na Chris Brown, pia Make It Rain ya Fat Joe na Lil Wayne.
Kanye West na Scott
Sasa comment ya kwanza ya Scott baada ya kuona hii post ya Lamar ni swali, Kwanini unaweka beat zangu kwenye Instagram yako? Lamar akamjibu… karibu kwenye ulimwengu wako boss, mimi ni shabiki wako mkubwa, endelea kutu-inspire, Scott akamjibu.. tafadhali naomba usipost beat zangu ukajidai ni wewe umezitengeneza.
Scott
Baada ya hapo Lamar alimjibu... ‘Hakuna matata boss, haitatokea tena‘ na Watanzania wengine wakaanza kucomment akiwemo producer Mtanzania Lucci, wasanii Dogo Janjana Julio Batalia.
Lamar ameongea na millardayo.com baada ya hii ishu na kusema baada ya hizi comments ilibidi amuandikie Scott msg private na kumueleza kwamba hakuwa na nia mbaya kwa alichokifanya, Scott alikuwa mpole na kuelewa nia ya Lamar… akamjibu ‘sawa kaka‘
Video aliyoipost Lamar ikiwa na hiyo beat ni hii hapa chini..
0 Response to "Producer Scott Storch wa Marekani hakupenda kuona Mtanzania Lamar kapost beat yake Instagram? tazama comments zake"