Madiwani wa Halmashauri ya Mbeya Vijijini wamegoma kupitisha kifungu cha bajeti ya kumnunulia mwanasheria wa halmashauri suti ya Sh500,000 kila mwezi.
Awali, akiwasilisha bajeti ya mwaka 2016/17 kwenye Baraza la Madiwani kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri Mbeya Vijijini, Mwanasheria Prosper Msivala alisema kila mkuu wa Vijijini, Mwanasheria Prosper Msivala alisema kila mkuu wa idara atapata Sh180,000 kwa ajili ya mawasiliano huku wanasheria wakipewa Sh500,000.
Msivala alisema suti ya mwanasheria ni pamoja na viatu, shati, suruali na koti pamoja na skafu yake.
Diwani wa Maendeleo Mbeya Vijijini, Daniel Mwanyamale alipinga mwanasheria kushonewa sare kila mwezi kwa Sh500,000.
Aliwataka waandaaji wa bajeti hiyo kuangalia upya suala hilo na kwamba hata suala la kupewa Sh180,000 za mawasiliano nalo halikubaliki.
Diwani Ramadhani Njelambaa alisema afadhali fedha hizo zipelekwe kwenye shughuli za maendeleo ukiwamo ujenzi wa madarasa na ununuzi wa dawa za vituo na zahanati. Hata hivyo, Mwanasheria Msivala alitetea fedha hizo akisema ni jukumu la halmashauri kutoa na kuwaomba madiwani wapitishe.
“Ndugu zangu kila mwanasheria anapoajiriwa katika halmashauri yetu ni lazima kila mwanasheria apate Sh500,000 na hilo lipo kisheria,” alisema.
Mbunge wa Mbeya Vijijini, Aran Njeza aliwasihi madiwani kuachana na mijadala ya posho katika vikao badala yake wajadili matumizi ya fedha zilizopangwa kwa miradi ya maendeleo ya wananchi.
GUSA HAPA CHINI KUWA MSHINDI
0 Response to "Madiwani Mbeya waigomea Shilingi 500,000 ya suti"