Frederick Mwakalebela Shitaka lake la Kupinga Ubunge wa Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) Wafutwa atakiwa kumlipa gharama msigwa.

Mr me 0 comments
Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imetupilia mbali kesi ya kupinga matokeo yaliyompa Ubunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), iliyofunguliwa na aliyekuwa mpinzani wake kwenye Uchaguzi huo, Frederick Mwakalebela (CCM).

Mahakama hiyo pia imeamuru Mwakalebela kumlipa Mchungaji Msigwa gharama za kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka jana na kupata usajili wa mahakama hiyo Novemba 30.

Katika shauri la msingi la kesi hiyo namba 5 ya mwaka 2015 ya kupinga matoke, Mwakalebela aliwatuhumu Mchungaji Peter Msigwa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Iringa Mjini, Ahmed Sawa kwa kukiuka sheria na taratibu za uchaguzi hali iliyopelekea yeye kupata matokeo mabaya yasiyo halali.

GUSA HAPA CHINI KUWA MSHINDI




Google+ Pinterest

0 Response to "Frederick Mwakalebela Shitaka lake la Kupinga Ubunge wa Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) Wafutwa atakiwa kumlipa gharama msigwa."

  • Commented politely and wisely in accordance with the content.
  • Comments are not needed by other readers [spam] will be removed immediately.
  • If the article entitled "Frederick Mwakalebela Shitaka lake la Kupinga Ubunge wa Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) Wafutwa atakiwa kumlipa gharama msigwa." is useful, share to social networks.
Code Conversion