Video queen Gigy Money ambaye hivi karibuni alikuwa kwenye vichwa vya habari za burudani baada ya msanii Tekno Miles kutoka Nigeria, kukana kuwa na mahusiano naye, amefunguka jipya na kuweka wazi watu ambao aliwahi kuwa na mahusiano nao.
Akiongea katika kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Television, Gigy alisema kuna baadhi ya wasanii alishawahi kuwa nao kwenye mahusiano akiamini watamtoa kimaisha, lakini ilikuwa kinyume na kuishia kuchezewa tu.
“Mimi nilishawahi kudate na Hemed PHD nikiamni atanitoa nitatoboa, lakini wapi, Hemedi alishawahi kugombana na Rich Mavoko kwa ajili yangu, tena kipindi hiko niko form two, unajua maisha kila mtu kuna aliyopitia, nilishawahi kuwa na mtu ambaye hata hatuendani lakini nilikuwa nalazimika, mtu ameshanimilikisha gari, nyumba, tukitoka nalazimika kuvaa angalau nifanane nae kiutu uzima”, alisema Gigy.
Akiendelea kuelezea harakati za maisha yake anasema pamoja na Rich Mavoko kugombana na Hemedi, lakini pia alishawahi kumuharibia kwenye mahusiano yake ambayo alikuwepo kwa wakati huo, na kumtaka kuacha tabia za kike.
“Richard akaharibu mahusiano yangu, Richard kama Richard aache tabia za kike”, alisema Gigy.
GUSA HAPA CHINI KUWA MSHINDI
0 Response to "Hemedy na Rich Mavoko Wamenigombania- Gigy Money"