Kwenye 255 XXL Clouds fm leo, stori zilizopata airtime ni pamoja na hii ya Nuh Mziwanda kueleza kuwa enzi za uhusiano wake na Shilole hakuweza hata kununua hata feni kwasasabu alikuwa akibanwa.
‘Ni kweli nilikuwa naishi kwa mwanamke wangu, lakini alikuwa hataki ninunue chochote, wazazi na ndugu zangu walinihimiza nijitambue kuwa mimi ni mwanaume lakini sikuzingatia‘ ;-Nuh Mziwanda
‘namuomba msamaha mama yangu na pia kwa wale wote waliokuwa wananipa ushauri , nilijua nimepata kumbe nimepatikana na sasa mimi nimekuwa Nuh mpya‘ ;-Nuh Mziwanda
Nyingine pia ni hii ya Ray Vicent Kigosi akizungumzia mpango wa kutumia maji kumuingizia mkwanja baada ya kumake headline kibao kwenye mitandao
‘Nimepata mawazo mengi kutoka kwa watu, naweza kufanya dokumentari ya nini umuhimu wa maji, nikawaelimisha watanzania kuhusu umuhimu wa maji na nikapata pesa‘ ;-Ray Kigosi
Baada ya headline kusambaa katika mitandao mbalimbali kuhusu kufungiwa kwa mdundo mpya wa Ay ft Diamond Platnumz ‘Zigo’ TCRA kupitia kwa Meneja Mawasiliano Innocent Mungy wanasema wamekanusha taarifa hizo na kusema ‘tumetoa taafira kwenda kwa watangazaji wa vitu vya Televisheni kubainisha maudhui yanayopaswa kuonekana haswa mchana wakati watoto wanaangalia Tv ‘
‘Taarifa tuliyoitoa ni kusitisha kurusha nyimbo zinazokiuka kanuni za utangazaji na za maudhui, kwa kuonyesha picha zisizo na maadili na kuchochea watoto kuiga maadili mabaya ‘ ;-Innocent Mungy
Full stori unaweza pia kuisikiliza kwenye hii sauti hapa chini…
GUSA HAPA CHINI KUWA MSHINDI
0 Response to "Video ya Ay ft Diamond Platnumz ‘Zigo’ kufungiwa? Ray Kigosi kutumia maji kuingiza mkwanja…? (255 +AUDIO)"