Hospital iliyomnasa usalama wa taifa Feki Yaanikwa

Mr me 0 comments

DAR ES SALAAM: Ile Hospitali ya Head 2 Toe Super Specialized ya Ununio Kunduchi, Dar ambayo ilimnasa jamaa aliyejipachika kazi ya usalama wa taifa na kutambulika kwa jina moja la Manase, (pichani) sasa mmiliki wake amejitokeza na kuanika kila kitu kuhusiana na hospitali hiyo.

Akizungumza na waandishi watu ofisini kwake, Ijumaa iliyopita, Dk. Paul Marealle ambaye ndiye mmiliki, alisema hospitali hiyo imesajiliwa kihalali kwa namba 071409 ya mwaka 2013 na kwamba wanaofanya kazi hapo ni wataalam wa viungo.

Aliendelea kusema kuwa, hospitali hiyo inatoa tiba ya viungo na mifupa ambayo ina wataalam, tofauti na inavyotafsiriwa kuwa haikuwa na kibali cha shughuli hizo.

“Hospitali ile ni yangu, pia imejiunga na Bima ya Afya mwaka jana. Kwa hiyo kwa ujumla haina tatizo lolote lile, iko safi kabisa na mtu anayeitwa Fortdas Fidell ni mtaalam wa viungo pale,” alisema Dk. Marealle.

Februari 10, mwaka huu, Manase na wenzake waliojiita kuwa ni usalama wa taifa walidaiwa kuomba fedha zaidi ya shilingi milioni 22 wakidai kuwa, hospitali hiyo haina wataalam wala usajili.

Simu ya madai hayo, ilimfikia mtaalaam wa viungo hospitalini hapo aitwaye Fidell ambaye alikutana na watu hao nje ya Chuo cha Usalama wa Taifa, Tegeta, Dar na kuwataka waongozane mpaka hospitalini wakachukue pesa hizi huku akiwa ameshawasiliana na mwenzake hospitalini hapo.

Walipofika, mwenzake huyo anayeitwa Ndonde alipia risasi juu baada ya kuwaona wale wa kwenye gari wakihaha kushuka kwa nguvu kabla ya kuingia ndani ya geti na waliposikia mlio wa risasi walikimbia na kumwacha Manase akiwa anashikiliwa na wafanyakazi wa hospitalini hapo mpaka polisi walipofika.

Gazeti la Uwazi namba 976 la Februari 16, mwaka huu lilichapisha habari hiyo kwa kichwa kilichosema; ALIYEJIPACHIKA CHEO CHA USALAMA WA TAIFA AKIONA!
GUSA HAPA CHINI KUWA MSHINDI

Google+ Pinterest

0 Response to "Hospital iliyomnasa usalama wa taifa Feki Yaanikwa"

  • Commented politely and wisely in accordance with the content.
  • Comments are not needed by other readers [spam] will be removed immediately.
  • If the article entitled "Hospital iliyomnasa usalama wa taifa Feki Yaanikwa" is useful, share to social networks.
Code Conversion